WATUMISHI WA CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI)

06 May, 2022
WATUMISHI WA CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI)

Watumishi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) wameungana na wafanyakazi duniani
katika kuadhimisha  siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) kimkoa katika
viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika maadhimisho hayo yaliyobeba kauli mbiu “Mishahara na Maslahi bora kwa Wafanyakazi ndio kilio chetu, Kazi Iendelee”, Wafanyakazi wa chuo cha bahari Dar es Salaam wameahidi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla hususan katika kusimamia na kuboresha sekta ya bahari kuelekea Uchumi wa Bluu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho hayo, amewataka wafanyakazi kuendelea kuchapa kazi wakati changamoto
zao zinaendelea kufanyiwa kazi na serikali ya awamu ya sita.

Watumishi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) wakiwa katika picha ya pamoja 
kabla ya kuanza safari kuelekea uwanja wa Uhuru ambapo sherehe za Mei Mosi
ziliadhimishwa kimkoa katika mkoa wa Dar es Salaam.

Watumishi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) wakiwa katika maandamano ya 
kuingia kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi
iliyofanyika kimkoa jijini Dar es Salaam.

Watumishi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla (Pichani hayupo pichani) alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi katika sherehe za Mei Mosi 2022 iliyofanyika katika viwanja vya Uhuru.